ROZARI YA BIKIRA MARIA MAMA WA MSAADA WA DAIMA

Virgin Mary of Perpetual Help-min

Namna ya kusali Rozari kwa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima
(Tumia rosari ya kawaida)


Mwanzo, kwenye Msalaba: Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

Kwenye chembe ndogo za awali:
K: Ee Mungu utuelekezee msaada; W: Ee Bwana utusaidie hima W: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Maria ametusaidia,Maria anataka kutusaidia,Maria anaweza kutusaidia,Maria atatusaidia. 

KATIKA KILA FUNGU SALI SALA ZIFUATAZO:
Kwenye chembe kubwa:
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,Kama mwanzo na sasa, na siku zote, na milele. Amina.
Maria ametusaidia,Maria anataka kutusaidia,Maria anaweza kutusaidia,Maria atatusaidia. Ee Maria Mama wa Msaada wa daimaSikiliza maombi ya roho zetuUnaweza kutusaidia katika mahitaji yetuEe Maria kwa matumaini twakuita wewe.

Kwenye chembe ndogo: (Kama unasali mwenyewe) “Ee Maria, utusaidie! (mara kumi). Kama mnasali zaidi ya mmoja kwa pamoja: K; Ee Maria,  W: Utusaidie. (mara kumi) 

MWISHO SALI SALA ZIFUATAZO:
Salamu Maria: Salamu Maria, umejaa neema,  Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu Mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa, na saa ya kufa kwetu. Amina. (mara tatu) 

Tunaukimbilia: Tunaukimbilia ulinzi wako, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe siku zote, kila tuingiapo hatarini, ee Bikira Mtukufu na mwenye baraka,. Amina.

Kusoma maelezo zaidi kuhusiana na picha,na historia ya Ibada ya Bikira Maria Mama Yetu wa Msaada wa Daima, bonyeza hapa.

Kupata kitabu chenye sala hii, bonyeza hapa.

Kupata bidhaa zingine kama picha, vitenge vya Java na Cotton, sanamu, n.k., za Bikira Maria wa Msaada wa Daima, bonyeza hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Main Menu