BIKIRA MARIA MSAADA WA DAIMA
(Our Lady of Perpetual Help)

msaada wa daima-min

Picha hii ya Bikira Maria Msaada wa Daima ni moja wa picha za zamani sana na inafahamika kwa kuleta uponyaji na kutenda muijuza mingi kwa wote iliopita mikononi mwao.

Historia kamili ya picha hii inaanzia karne ya 15. Picha hii ilikuwa ikitunzwa katika monasteri moja katika kisiwa cha Krete, Ugiriki (japokuwa kipindi hicho tayari ilikuwa ikitunzwa kama picha za kale).

Mnamo mwaka 1495 palikuwa na tishio la uvamizi wa jeshi la Uturuki (jeshi kutoka utawala mkubwa zaidi kipindi hicho). Picha hiyo ilichukuliwa na bwana mmoja mfanyabiashara, mpaka nyumbani kwake, huko Roma, Italia. Mara tu baada ya kufika nayo nyumbani aliugua ghalfa, na katika dakika zake za mwisho alimuomba rafiki yake aiwahishe picha hiyo katika moja ya kanisa huko Roma ili ibada yake iendelee.

Rafiki yake aliichukua kwa nia hiyo, ila mkewe alimsihi akimtaka wakae nayo nyumbani. Basi walikubaliana hivyo na ikakaa kwao kwa miezi mingi kidogo. Siku moja usiku Bikira Maria alimtokea ndotoni huyu bwana na kumuonya kuwa asikae nayo hiyo picha kwa kuwa si mali yake, ni mali ya kanisa, na aipeleke kanisa, lakini hakutilia maanani. Alimtokea mara mbili zaidi, ila mara ya tatu alimuonya kuwa asipoipeleka atakufa kifo kibaya sana. Bwana huyu alipoamka alishauriana na mkewe kuipeleka kanisani, ila mkewe akamwambia ni hofu tu. Bikira Maria alimtokea tena, akamwambia kwa sababu amekaidi, basi adhabu yake yaja. Na ndani ya muda mfupi aliumwa sana na kufariki.

Bikira Maria alimtokea tena mtoto mdogo wa kike wa miaka sita (6) wa huyu Bwana aliefariki na kumwambia amwambie mama yake kuwa; “Bikira Maria anakuamuru umtoe ndani ya nyumba hii”. Mama kusikia hivyo, akakumbuka pia na ndoto za marehemu mumewe, aliogopa sana na akawa anaelekea kuipeleka kanisani. Ndipo ‘shoga ake’ (jirani yake), akamuomba sana kuwa aendelee kuitunza kwani ni ya thamani sana, na ile ni ndoto tu, haina ukweli wowote.

Basi mama wa watu alielewa somo, na kurudi nayo nyumbani. Usiku ule ule, yule jirani (shoga ake) aliugua sana, ndipo alipotambua kosa lake na kumsihi Bikira Maria kuwa atahakikisha picha inafika kanisani siku inayofuata, na akapona papo hapo.

Bikira Maria alimtokea tena yule mtoto wa mama mwenye picha na kumwambia amwambie mama yake kuipeleka picha ile kwenye kanisa lililopo katikati ya kanisa la Bikira Maria Mkuu na lile la Mt. Yohana Lateran. Ndipo kulipokucha, tarehe 27 Machi, 1499 picha hiyo ilipelekwa na kwenda kukabidhiwa katika kikanisa kidogo cha Mt. Mathayo mtume. Kikanisa kilikuwa kidogo sana, lakini hilo halikuwa kizuizi cha Bikira Maria kuonyesha ukuu wake. Kipindi wanaaingiza kanisani, mtu mmoja alikuwa amepooza (paralysed) aliponywa hapo hapo na kuwa mzima tena.

Miujiza mingi sana iliendelea kutendeka pale, na ibada yake ikakuwa na kuenea duniani kote hata leo.
Kwa sasa picha hii ipo kwenye kanisa la Mt. Alphonsus, Italia. Huko Novena yake husaliwa kila wiki.

Picha na Vitenge vya Bikira Maria Msaada wa Daima unazipata hapa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Main Menu