Bikira Maria Mfungua Mafundo (Virgin Mary Untier/Undoer of Knots)

mfungua mafundo

Ibada kwa Bikira Maria Mfungua Mafundo ina zaidi ya miaka 300 japo imekuja kufahamika na kuenea sana kipindi cha uongozi wa Papa Francis I, na kipindi akiwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires, Argentina.
Papa Francis aliiona picha ya Bikira Maria Mfungua Mafundo na kuifahamu ibada yake kipindi yupo masomoni Ujerumani, katika kanisa la Mt. Petro (i.e., St. Peter am Perlach) na kuieneza kwa nguvu aliporudi Latin Amerika na sasa dunia nzima.

Historia ya Ibada ilianza hivi:

Bwana Wolfgang Langenmantel na mkewe, Sofia walikuwa na mpasuko mkubwa katika ndoa yao, iliyokuwa imebakia kidogo tu ivunjike.
Bwana Wolfgang alikuwa na mashaka makubwa sana kuhusu uhai wa ndoa hiyo na akawa anaenda kwa Padre Jacob Rem mara kwa mara kwa ushauri ambapo pia walikuwa wamejiwekea utamaduni wa kumwomba Bikira Maria kila wanapokutana.
Siku moja tarehe 28 Septemba, 1615 alipokwenda kuonana tena na Padri Jacob, Bwana Wolfgang alikuja na kimkanda walichofungwa siku ya ndoa, yeye na mke wake kama ishara ya umoja (i.e., wedding ribbon) kisha akampatia padri.
Padri Rem aliupokea na kisha akausimamisha karibu na picha ya Bikira Maria na kuomba;

“Bikira Maria tunakuomba ufungue Mafundo haya katika ndoa ya Wolfgang.”

Kamba hiyo ililegea papo hapo na kujifungua, na kisha kuwa nyeupe pe.
Mengi yaliendelea na kubwa zaidi ndoa yao ilipata kibali kwa Mungu na kuwa na amani tena. Wazungu wanasema; “and they lived happily ever after.”

Historia ya Picha ilikuwa hivi:

Mjukuu wao (Fr. Hieronymus Langenmantel) ambae alikuwa na kuwa padri, aliomba picha ichorwe kukumbuka tukio hilo kubwa.
Ndipo picha hiyo nzuri ilichorwa na Johann Georg Melchior Schmidtner miaka ya 1700’s inamwonesha Bikira Maria akiwa amesimama juu ya mwezi na kumkanyaga nyoka/shetani (kuwakilisha Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili). Pia kazungukwa na malaika (mmoja akiwa anampa kamba iliyo na mafundo na mwingine akiipokea kamba iliyokwisha funguliwa mafundo), Roho Mtakatifu katika umbo la njiwa na akiziangazia taji la nyota kichwani mwa Bikira Maria.
Chini kabisa ni Mt. Rafaeli Malaika Mkuu akimuongoza Wolfgang kuingia monasteri.

“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke. Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu…” (Ayubu 14:1)

Matatizo ni sehemu ya maisha, hata uwe unamjua na kumpenda Mungu kiasi gani, changamoto za hapa na pale haziwezi kukosa.
Yapo matatizo tunayoyasabisha sisi wenyewe kulingana na namna tunavyoingiliana na walimwengu, kwa nia nzuri na mbaya. Na yapo mengine hutupata sababu ya wengine. Lakini tunaambiwa tuyapokee yote kwa saburi.

Katika maisha kuna matatizo ambayo ni magumu na mazito sana, na hatuwezi kuyatatua kwa akili zetu wenyewe au sala za kawaida.
Na hapa ndio tunamwangukia mama yetu mpendwa kupitia ibada yake ya Bikira Maria Mfungua Mafundo. Tatizo liwe gumu vipi, tukimkabidhi Mama Maria linakuwa si gumu tena.
Vifungo vyetu ambayo tumeshindwa kuviacha kwa muda mrefu kama ulevi, uongo, ulevi, mangonjwa yasiyoponywa, manyanyaso katika ndoa, kufungamanishwa na nguvu za giza, n.k.
Hizi zote na nyingine nyingi ni misalaba ambayo ni budi kumkabidi Mama kupitia ibada hii kubwa, naye hufungua vifungo hivyo na kufanya maisha kuwa matamu tena.

Unaweza nunua kitabu chenye ibada ya Bikira Maria Mfungua Mafundo kwa ku-click hapa.

Pia picha nzuri za sizes mbalimbali kwa ajili ya ibada hii zinapatikana hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Main Menu