Karibuni PHILOMART
Kupitia PhiloMart wakatoliki na wakristu mbalimbali Tanzania na Afrika Mashariki kulingana na mahitaji yao ya sala, elimu, visakramenti, vifaa vya nyimbo na ibada, mavazi ya watawa, watumishi wa altare, wanakwaya, wasoma masomo, n.k., wanakutanishwa na wakristu wenzao wanaotengeneza na kusambaza bidhaa husika kupitia mtandao, bila kujali wilaya, mkoa au nchi walizopo.
Duka hili la mtandaoni linakuwezesha wewe muumini uliepo Bukoba, Mombasa, Mafia (au popote pale duniani) kununua bidhaa yoyote ile ya dini kwa ajili yako au mpendwa wako kutoka maduka ya Dar es Salaam na kufikishiwa siku hiyo hiyo au inayofuata bila kutembea hata hatua moja (umbali si kikwazo tena).
“Uaminifu, Uharaka, Ubora na Unafuu ndio kauli mbiu zetu.”
Tunakuwezesha kununua bidhaa yoyote ya dini kupitia website yetu, na kukamilisha malipo yako kwa M-PESA, TIGOPESA, VISA, MASTERCARD, BANK DEPOSIT na CASH ON DELIVERY (Unalipia baada ya kupokea mzigo). Njia zote ni salama na rahisi zaidi kwa kutumia simu/computer yako.
Kwa Dar es Salaam unaweza pokea mzigo wako ndani ya masaa 24, ila kwa mikoani ndani ya masaa 24-48.